TLA inawaalika wakurugenzi, mameneja, wakuu wa vitengo na wataalamu wa maktaba na taarifa kwenye mafunzo ya siku tatu ya uongozi jijini Arusha, 24–26 Novemba 2026.
Chama cha Maktaba na Taarifa Tanzania (TLA) kinawaalika Wakurugenzi, Mameneja, Wakuu wa Idara, Sehemu na Vitengo, pamoja na Wataalamu wa Maktaba na Taarifa, kwenye mafunzo mahususi ya maendeleo ya kitaaluma kuhusu Uongozi wa Kimkakati katika Zama za Wingi wa Taarifa, kuanzia tarehe 24 hadi 26 Novemba 2026 katika Parrot Hotel, Arusha.
Katika mazingira ya sasa ya taarifa yanayobadilika kwa kasi, uongozi bora unahitaji fikra za kimkakati, maamuzi thabiti, utawala imara na uwezo wa kukabiliana na wingi wa taarifa.
Malengo ya mafunzo
- Kuimarisha uwezo binafsi wa uongozi.
- Kuboresha taratibu za utawala bora wa taasisi.
- Kujenga uwezo wa uongozi wa kimkakati ili kukabiliana na changamoto mpya za kitaasisi.
Ada ya usajili
- TZS 400,000 – Wanachama wa TLA
- TZS 500,000 – Wasio wanachama
Lipa kupitia NBC, jina la akaunti Tanzania Library Association, namba ya akaunti 0221030004145.
Maulizo: +255 756 170 340 / +255 772 286 363
Jisajili sasa na uhakikishe nafasi yako – maelezo kamili na fomu ya usajili yapo kwenye ukurasa wa mafunzo.

